March 2021
Mchungaji Mzinga azindua Youth Bible Club
Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kanisa Kuu Azaniafront, Mchungaji Charles Mzinga mnamo tarehe 1 Agosti 2020 alifanya uzinduzi wa klabu ya vijana ya usomaji na kujifunza biblia ijulikanayo kama Azaniafront Youth Bible Club (AYBC). Kuanzishwa kwa klabu hiyo kunalenga kuwapa fursa vijana wa Azaniafront kusoma, kuchambua, kujadiliana na kujifunza biblia kwa kina.
Azaniafront Cathedral - Ratiba ya Ibada za Pasaka 2021
Mpendwa msharika na watu wote wa Mungu, hii hapa ni ratiba ya ibada zetu katika msimu huu wa sikukuu za Pasaka za mwaka 2021. Unakaribishwa kuhudhuria misa takatifu hapa usharikani. Pia unaweza kufuatilia ibada hizi kwa ukaribu ukiwa mahali popote duniani kwa kuangalia LIVE kupitia chaneli yetu ya YouTube ya AZANIAFRONT TV.
Karibu sana na Mungu akubariki.
01/04/2021: Alhamisi Kuu - Ibada mbili
* Ibada ya Kiingereza: Saa 11:00 jioni
* Ibada ya Kiswahili: Saa 01:00 usiku
